CURRENT NEWS

KITAIFA

Siasa

MICHEZO NA BURUDANI

Monday, August 3, 2015

YALIOTAWALA KWENYE MAGAZETI YA LEO, AGOSTI 3
NAPE AONGOZA KURA ZA MAONI


Sunday, August 2, 2015

MTOTO WA MAMA NTILIE JUMAA AWESO ASHINDA KWA KISHINDO UCHAGUZI WA NDANI CCM PANGANI


aweso
Ndugu Jumaa Aweso.
Na Mohammed Hammie, Pangani, Tanga
Mtoto wa mama ntilie mwenye uzao halisi kutoka wilayani Pangani mkoani Tanga, Ndugu Jumaa Aweso (pichani) ameibuka na ushindi wa kishindo katika uchaguzi wa ndani wa chama cha mapinduzi CCM.
Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo katibu wa CCM wilayani Pangani Bi Zaina Mlawa amesema kuwa, katika uchaguzi huo uliowashirikisha wagombea wapatao kumi na moja, Ndugu Aweso amekuwa wa kwanza miongoni mwa wagombea hao.
Uchaguzi huo uliokuwa na ushindani wa aina yake kutokana na kuwepo kwa aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo Ndugu Salehe Pamba, uliwashirikisha wapiga kura wapatao 10376 wa chama cha mapunduzi.
Awali wakati akitangaza matokeo ya uchaguzi huo, Bi Zania aliwataja wagombea hao kwa idadi ya kura walizopata na kusema kuwa "Ndugu Wahi Ibrahim amepata kura 87, ndugu Rosemary Luanda amepata kura 89, ndugu Elizabeth Alatanga amepataa kura 158, Halima Kimbau amepata kura 222, Ndugu Mohammed Rished amepata kura 442, Ndugu Ayubu Mswahili amepata kura 565"
Bi Zania ameongeza kwa kusema kuwa "Ndugu Omary Mwidadi amepata kura 587, ndugu Omary Chambega amepata kura 720, ndugu Salehe Pamba amepata kura 1567, ndugu Abdurahmani magati amepata 1956, na ndugu Jumaa Aweso 3983"
Ushindi huo kwa ndugu Jumaa Aweso unampa nafasi ya kuwa mgombea wa kwanza katika kuipeperusha bendera ya chama cha mapinduzi CCM wilayani Pangani endapo kamati kuu ya maamuzi itaridhia.
Mpaka sasa katika jimbo la Pangani kumepatikana wagombea wawili ambao wanaonekana kupendwa sana na wanancho ambao ni Amina Mwidau wa CUF pamoja na JUmaa Aweso wa CCM ambapo kwa mujibu wa wachambuzi wa masuala ya siasa, endapo watakutana katika nafasi ya ubunge upinzani utakuwa wa aina yake.

MAGAZETI YA LEO TZ,KURASA ZA MBELE NA NYUMA,AUG 2

Saturday, August 1, 2015

MIUJIZA MALI KWENYE UKUTA,WENGI WAVUTIWA

Maelfu ya raia katika mji mkuu wa Mali Bamako wanaendelea kufurika ili kujionea kile kilichotajwa kuwa muujiza wa kidini katika ukuta mmoja ambao ulionekana wikiendi iliopita.
Wengi wanaamini picha hiyo nyeupe katika ukuta wa nje wa choo inamuonyesha mtu akisali na kuonekana kama ishara ya ujumbe wa Mungu.
Maafisa wa polisi wa kukabiliana na ghasia walipelekwa katika eneo hilo ili kudhibiti umati huo kwa kuwa watu wanapiga foleni usiku kucha kuona muujiza huo wa alama.
''Tunaamini ni maono ya mtume wetu'', Aliou Traore ambaye anaishi katika eneo hilo aliiambia BBC.
mali
''Watu wamekuja kutoka Senegal kujionea huku baadhi ya mawaziri wa Mali pamoja na viongozi wa dini wakitutembelea kuona muujiza huu'',alisema.
Bwana Traore amesema kuwa alama hiyo imekuwa ikibadilika tangu ionekane mara ya kwanza.''Mara nyengine alama hiyo inajifuta na kuonekana katika maeneo mengine ya nyumba hizi.Baadaye inarudi'',alisema.
Mwandishi wa BBC Alex Duval Smith mjini Bamako anasema kuwa watu hawalipi chochote kuona alama hiyo lakini wanawacha fedha katika ndoo,ambazo familia ya Traore inasema itazitoa kwa msikiti wa eneo hilo.
Wakati ripota wetu alipotembelea eneo hilo,alama hiyo ilionekana kama kovu la simiti la mwanamke aliyesimama.Picha za alama hiyo zimesambaa mjini Bamako kupitia simu tangu ionekane siku ya jumamosi.
Mali
''Ni muujiza ,nimeuona'',alisema mwalimu wa shule ya msingi Aboubakar Diarra baada ya kuona ukuta huo.''Ni kweli.Ni alama kutoka kwa Mungu kwa Mali .taifa letu ni kubwa''.
Wafuasi wa Tijani ambao hupatikana magharibi mwa Afrika wanajulikana kwa kuheshimu miujiza.

MWANZILISHI WA FACEBOOK KUWA BABA

Mwanzilishi wa mtandao wa facebook Mark Zickerberg na mkewe Priscilla Chan wanatarajia mtoto wa kike.
Wawili hao walitangaza katika ujumbe wao katika ukurasa wa facebook wa bwana Zuckerberg, ''Priscilla na mimi tuna habari njema:''Tunatarajiwa mtoto wa kike'', aliwaandikia takriban watu milioni 33 wanaomfuata katika mtandao huo.
Katika ujumbe wake Zuckerberg mwenye umri wa miaka 31 alifichua kwamba mkewe aliharibikiwa na mimba mara tatu hapo awali,lakini akongezea kwamba hatari ya kuharibikiwa na mimba nyengine kwa sasa iko chini sana.
Amesema kwamba wameamua kutoa tangazo hilo ili kuwapa watu wanaokabiliwa na tatizo kama hilo motisha wa kuendelea kuwa na subra

WAANDISHI WA HABARI WATAKIWA KUWA MAKINI NA HABARI WANAZORIPOTI


YALIYOTAWALA KWENYE MAGAZETI YA LEO TZ,AUG 1
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania