Tupunguze hadithi................
Takribani miaka miwili sijaandika makala wala kufikiria kama ninge andika tena ila nimeona kuna umuhimu wa kuandika hata kama zitakuwa na chembe chembe za lawama............miezi miwili imeshapita tangia nimerudi kwenye jiji la Dar es salaam, kwanza nimegundua kuna mabadiliko mengi sana, kuna vitu vingi sana vipya na watu wamefurika sana........nachoona kwa macho yangu mawili kwamba kusipofanyika maarifa ya haraka taifa litapunguza nguvu kazi...watu wamekaa kuongea na kuongea kwenyewe ni mada zisizojenga,Tv nyingi zinaonyesha mambo ambayo yanaharibu moja kwa moja watoto na hii ni hatari kwa Taifa...Uvivu ndio suala kubwa watu wanataka pesa bila kuzifanyia kazi kila saa kuomba omba ,utasikia bro 'unajua ndugu yako mchana sijauona'Ukimpeleka kazini nako hakosi sababu mara kazi ngumu mara mshahara unachelewa...unataka ulipwe kirahisi bila kuzalisha hizo pesa za kulipwa zitatoka wapi kama hauzalishi?
Kitu kingine kinachosumbua ni kuona watu hawana wema ..wenye Taxi na Bajaj ugomvi...wahudumu hawana lugha nzuri kwa wateja.....kuhalalishwa lugha za matusi,yaani kila mtu anatukana na wala hastuki kuwa anavunja sheria, anaona ana haki ya kutukana...............hali hii ikiendelea sijui tutajenga taifa gani miaka ijayo inabidi tubadilike ..turudishe upendo na umoja.

1 Comments:
Nakubaliana na ww kwa namna moja au nyingine watanzania wamezidi uvivu,cio tuu wa kufanya kazi hata wa mawazo, inabidi mabadiliko yafanyike haraka ili tuweze kuendana na dunia hii ya leo!....bila hivyo maendeleo ya nchi yetu yatachelewa kufika!...
Post a Comment
Subscribe to Post Comments [Atom]
<< Home